KUWA MASHAHIDI WAAMINIFU



KUTUMIKA KATIKA ULIMWENGU



UNAOBADILIKA



Lakini wakati roho mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata mwisho wa dunia. (Matendo: 1:8 ).



Kijitabu cha usomi kama

Matayarisho ya mkutano mkuu wa



21 wa FWCC



Kings College

Auckland

Aotearoa/New Zealand



Kuanzia tarehe 16-25 Januari 2004







Friends World Committee for Consultation

4 Byng Place, London WCIE 7LE, UK















Matumizi ya kijitabu hiki



Kuwa mashihidi waaminifu: kutumika Mungu katika ulimwengu unaobadilika ndio kiini cha Mkutano Mkuu wa 21 wa FWCC. Ni mwaliko wa kuleta pamoja njia za kufuata mwito wa pamoja katika tamaduni zetu tofauti,ujuzi na desturi za Marafiki.



Kijitabu hiki kina madhumuni ya matumizi kwa wale Marafiki wanao jiandaa kuhudhuria Mkutano Mkuu, kwa vikundi vya Marafiki wanao waakilisha, na kwa Marafiki katika mikutano ama makanisani popote. Kijitabu hiki kina sura kumi na nne za maono juu ya kiini cha Mkutano Mkuu kutoka kwa tamaduni tofauti za Marafiki kila tamshi la dhabiti limetokana na ujuzi wa wahusika wa jamii ya kimataifa ya Marafiki,kila mhusika akitaafuta uaminifu kulingana na mwanga wake. Mkutano Mkuu wa FWCC na kongomano za ulimwengu hutoa nafasi dhati ya kuabudu pamoja, kusikiza na kujuliana hali kwa nini kuwa Rafiki. Kijitabu hiki ni mwelekeo wa kuhusika kwa nafasi hiyo. Tunapojifunza kuhusu ujuzi wa kila mmoja wetu kuhusu Mungu jukumu letu sikuhukumu, bali ni kutokana na kimo cha ukweli wa peupe wa dada na ndugu zetu. Pengine kitapanua hisia zetu kuhusu maana ya kuwa Rafiki.



Taarifa hizi zimtolewa ili zisomwe na kufikiriwa na kila mmoja kwa vikundi vyenu. David Blamires mhariri wa jaride liitwalo Friends Quarterly na aliye mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa Marafiki ulimwenguni kule Britain Yearly Meeting, amehariri na kutupangia taarifa hizi. Tuna imani kwamba maswali yajayo baada ya tahariri hizo yatakuwa ya msimamo wa kibinafsi ya mawazo ya pamoja. Tunapendekeza kwamba uchague taarifa yenye tamaduni tofauti kulingana na imani yako ya Marafiki. Masomo haya yatawasaidia wawakilishi kwa mkutano mkuu kujihami na ujuzi. Vikundi vya ibaada kaika mkutano mkuu vina himizwa kuwa na fursa yakutosha ya kulinganisha kiini cha mkutano mkuu na taarifa na maswali yaambatanayo.



Octoba 2002 Kamati ya mipango ya kimataifa



Fahisiri



Ukurasa



Utumiaji wa kitabu hiki 2



Kumngojea Mungu kwa uaminifu

David Blamires Britain YM 4



Ushahidi Elizabeth Yano Bware YM



Hadithi ya Nadia Max Carter N. Carolina YM (FUM)



Mhuduma wa Mungu Angella Beharie Jamaica YM



Ushihidi kwa uaminifu Rachel Muers Britain YM



Ujumbe wa Marafiki Helmer Batista N.Carolina YM (FUM)



Ukweli usiyobadilika Phyllis Short Aotearoa/New Zealand YM



Thibitisho Susanna Brindle Australia YM



Moto mioyoni mwetu Diego Chuyma INELA Bolivia



Ushahidi Anne Thomas Canadian Y M



Kutangaza habari njema Dan Cammack Northwest YM



Kesha Kwa amani Misha Roshchin Moscow M M



Ushahidi uaminifu Kenneth Co Hong Kong M M



Kujenga Msingi wa uaminifu wa amani

Val Liveoak South Central YM





Kumngojea Mungu kwa uaminifu



David Blamires (Mhariri) Britain Yearly Meeting



Ni jambo la kufurahisha kwangu kupata nafasi hii ya kuhariri mchango huu wa maandishi kuhusu kiini cha mkutano mkuu, Kuwa mashihidi waaminifu: kutumika Mungu katika ulimwengu unaobadilika.. Kila mwandishi ametoa mchango wake kulingana na ujuzi wake wa kipekee wa tamaduni za msingi wa marafiki na shukurani za upendo na himizo, ugunduaji na maswali. Tunatoa shukrani zetu kwa itiko la upelelezi wa kiini cha mkutano mkuu. Ni tarajio langu kwamba kila msomaji ataweza kusikiza sauti ya Roho Mtakatifu kupitia maandshi ya kila mwandishi kwa kuwa yote ni changa moto kwetu sisi sote.

La ajabu kwangu ni kugundua kwamba tuna umoja wa dhati. La umuhimu kwetu ni ushirika wa kila mmoja kwa kutafuta amani na haki na kiri za uaminifu, urahisi na usawa. Haya ni matunda ya uaminifu wa kumngojea Mungu. Yesu yuatuambia, "Ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu" utaridhiwa na wale waliolisha wenye njaa, walio wapa wenye kiu kinyuaji, walio karibisha wageni, walio valisha wenye uchi na walio tembelea wagonjwa na wafungwa (Matayo 25: 31-40). Watakao kosa kutimiza haya watavuna lawama.

Haya ni changa moto ya maisha ya kila siku. Ingawaje wengine wataitwa kumhudumia Mungu katika sehemu za mbali na za aina ya majaribio, wengi wetu tumeitwa kuwa mashahidi waaminifu pale pale tulipo, kazini mwetu, katika jamii zetu na uajibikaji na ushirikiano wa dunia na vyote vya uhai vilivyomo. Uhai ni jambo kubwa mno kwa kila mtu kutengeneza mchango wake, lakini ni kubwa zaidi kwa kila mmoja wetu kufanya kila kitu. Tunahitaji kudhamini wenzetu kwa vipawa vinavyo tofautiana vya maono, kutambua kwamba tu washiriki tofauti wa mwili mmoja, kila mmoja na kazi yake. (Waroma 12: 1-21).

Mwaka wa 2002 ni mwaka wa ukumbush wa miaka 350 tangu uanzilishi wa dheheb la Marafiki, kiwanda cha uchapishaji cha kifalme kule Uingereza kili chagua kazi ya Elizabeth Fry ya mageuzi gerezani na kuweka picha yake kwa noti ya paundi tano pesa za Uingereza. Mwanzoni alipoongozwa kufanya kazi hiyo, Elizabeth Fry hakukuwa na uhakika na pia akawa na hofu, lakini akawa mwaminifu kwa kiongozi wake. Nasi kwa zamu yetu tumeitwa kuwa waaminifu kwa kazi Mungu ametuandalia. Ni kazi ambazo hatutakamilisha maishani mwetu.



Ushahidi



Elizabeth Yano Bware Yearly Meeting



Yesu aliahidi wanafunzi wake kwamba watapokea nguvu za kuwa

mashahidi baada ya kupokea nguvu za Roho Mtakatifu. Nguvu hizo zingehusisha ushujaa, uhodari, matumaini, ufahamu uwezo na mamlaka. Wanafunzi walihitajika kuwa na vipawa hivyo vyote ili waweze kukamilisha ujumbe wao.

Mungu ana kazi maalum anayo taka tumfanyie. Mambo mengi yaliotabiriwa na Yesu yanatendeka. Kuna mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ambayo yamesababisha shida kama: ufisadi, gharama ya kusema ukweli, ukavu, njaa, maasi katika siasa, vita vya kijamii na kitaifa, ndoa zinazovunjika, maboma yaliyo hamwa, mauaji, ufukara wa hali ya juu, uchafuaji wa mazingira kupitia viwanda, kilio cha umwagikaji wa damu, watu wanaotafuta amani.

Sisi kama wafwasi wa Kristo tuwe mashahidi kwa kueneza injili ya kristo kuhusu amani. Amani hutoka kwake nasi tuiendeleze. Ushuhuda wetu Marafiki ni kutafuta amani, kufuata utakatifu na maarifa ya Mungu, kutafuta uzuri unao sababisha amani kwa wote.

Roho ndani yetu atatuongoza kwa hali ya msamaria, yakutunza wageni na wahitaji. Dini ya kweli hufikiria matakwa ya mwanadamu na umoja wa utu.

Tukisha safishwa na nguvu za Roho Mtakatifu, twalazimishwa na injili kutoa wakati wetu, fedha zetu na huduma. Watu wengi hawana ufahamu mwingine ila uchungu wa kifo, ufukara, kutojua na songamano ya maumivu. Maisha yetu yaonyesheRoho wa Mungu yu ndani yetu. Imani na uaminifu viwe na mikono na mguu. Dini safi na ya kudumu machoni pa Mungu ni Kutunza mayatima na kuwajulia hali kwa shida zao, na kukataa kufanywa mfisadi na ulimwengu.

Kitabu cha Yona (3: 1-10) kinatoa hesabu ya taabu za mji wa Ninawe, Wakati Yona alitangaza ujumbe wa Mungu kwao. Kutambua Mungu kwa ghafula na watu wa Ninawe na viongozi wao ulifanya Mungu kukutana na kubadilika kwao kwa neema. Mtunga Zaburi kwa sala za toba alitambua kwamba masharti ya kutakaswa ni roho iliovunjika na moyo uliombondeka (Zaburi 51:17).

Maswali:

- Wewe na mimi twajihusishaje kuwa mashahidi kupitia wakati, fedha, mali, huduma na maneno yetu?

- Kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mbele ya Mungu kuhusu vile tumetumia ushuhuda, kipawa na huduma tulonayo. Wewe ni mleta amani au ni mwenye kuleta taabu?



Hadithi ya Nadia



Max L. Carter North CarolinaYearly Meeting (FUM)



Nyumba yao Nadia ilikuwa imeharibiwa na risasi za bunduki kutoka

kwa gari ya zana za vita usiku uliotangulia, naye na mumewe na watoto wao wadogo watatu walishikwa na hofu hata wakajikunyata kwa sakafu ya chumba cha kulala. Baada ya muda wa saa chache nilisimama na kikundi cha Wamarikani uwanjani mliokuwa na nyumba ya kipalistinia ilio kuwa imeharibiwa zaidi, na nikisikiza hadithi yake.

"Kwa muda wa nusu saa tulikuwa vitani vikali, na wanatuita wadhalimu! Hatuna bunduki, lakini ghari la mzinga lilikuwa likiturushia risasi katikati ya usiku, na wanatuita wadhalimu! Tulipofagia maganda ya risasi kutoka kwa nyumba yetu, tuliona yalikuwa yamewekwa mhuri, "Ilitengenezwa Umarikani". Natumai Wamarikani wote watateketea jehanum!"

Tungalifanya nini? Kama wafanya kazi wa kambi ya kujitolea wa shule ya Marafiki ya Ramallah wakati wa hali ya mwaka wa 2001, tulikuja kwa eneo hili kutoa ushahidi wa amri za bibilia kuhusu upendo na kuhudumu. Lakini ushahidi wetu ulikuwa umebadili maana kwa kuwa tulishuhudia uhasama na hasira. Kikundi chetu kilipokuwa kinashughulika na kazi ya jioni hiyo shuleni, hisia sahihi ya kuendelea ilitujia. Wakili wa amani katika Israeli na Palestina walikuwa wametuambia kwamba, kila mme au mke wa Kimarikani na hata mtoto walikuwa wakichanga wastani dola za Kimarikani 20 kila mwaka ili wanunue vyombo vya kijeshi ambavyo vilileta mvurugo katika sehemu hiyo. Kupitia mfano huo wa uchangishaji tulipeana kiasi hicho hicho cha dola za Kimarikani 20 kwa jamii ya Nadia kuwawezesha kukarabati nyumba yao. Kiwango hiki cha fedha kiliongezeka zaidi baada ya kujumlisha na zile zilizotolewa na Marafiki wa Kimarikani za kusaidia kazi ya dharura. Siku ilio fuata mwalimu wa shule ya Marafiki aliye mjua Nadia alitumwa kumpelekea fedha hizo tukatarajia atazipokea.

Baada ya siku chache tukiwa kwa nyumba ya mwalimu tukila chakula cha jioni, Nadia alipiga simu akiuliza kama angeweza kuleta jamii yake ili tuwaone. Tukawa na hamu ya kuwaona na kwa hali hiyo yamshangao! Angekuwa bado ana hasira?

Angechukulia zawadi yetu kama "Pesa ya damu?" Hofu tuliokuwa nayo ikapunguka. Nadia na jamii yake wakastarehe na kutushukuru sana. Baada ya muda mchache wa maongeo ya furaha, akauliza, "Marafiki ni wa Kristo?" Nilicheka na kumwelezea ya kwamba, katika sehemu zingine za Marafiki, swala hili laweza kuchukua saa nyingi kujibiwa. Hata ingawa tulikuwa na walakini tulijibu swali - "ndio". "Nilifikiria hivyo" akasema, kisha mwanamke mwisilamu akatoa kwa mkoba wake zawadi za kikristo na kutugawia: alama za msalaba kutoka Yerusalemu, msalaba wa mpigani wa kikristo, sanamu za Bethlehemu.

Hapo awali dalili za uadui zilikuwa kwetu: jamii ya Kipalestinia ya dini ya Ki isilamu ilikuwa imeharibiwa na wakristo wa Kimarikani na sisi wageni kutoka Umarikani. Lengo letu la awali la "kuwa mashahidi" kwa upendo wa Mungu kupatia huduma kwa wengine ilidhihirika ya kwamba ujuzi tulikuwa nao kuhusu ushuhuda wa uchungu ulihitaji mapatanisho.

Ujumbe wa Mungu wa uwezekano wa mapatanisho ulionekana: zawadi ya upendo ya alama ya msalaba iliopeanwa na Mu Islamu kwa Mkristo. Inawezekana kuwa ni mimi Rafiki wa pekee anayejua yeye anayebeba alama ya msalaba popote aendapo. Ni ukumbusho wa kila siku wa kweli kuhusu upendo wa ukombozi.

Maswali:

- Tunafanya nini kuweza kuelewana na jamii za imani ilio tofauti na yetu?

- Tunafanya nini sisi kama raia ikiwa serikali yetu inatuongoza kwa mashauri tunasadiki ni mbaya?

- Unajisikiaje mtu anapo onyesha ana hasira?



Mhuduma wa Mungu



Angella Beharie Jamaica Yearly Meeting



Tukiwa wahuduma wa Mungu lazima tujenge imani yetu kwenye "Nuru" inayoambatana na utaratibu wa Mungu ambao haupunguki kamwe. Imani ya Abrahamu kwa Mungu ilidhirihika kwamba alikuwa tayari kumfanyia Mungu chochote. Alikuwa mwaminifu kwa Mungu naye Mungu akaitakasa imani yake (Mwanzo 22:1- 8).

"Kwaini Mungu ndiye afanyaye kazi daima ndani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mipango wake mwenyewe" (Wafilipi 2:13). Ninasadiki kwamba Mungu ndio chanzo cha uwezo wangu na yumo ndani yangu kufanya hivyo? Kwa hivyo yanipasa kutii Roho Mtakatifu atakaye niwezesha kufaulu kuwa na uwezo wake kamili na sichengine hata. Ikiwa Mungu amenichagua kuwa chombo cha kufanya kazi, yanipasa kujitoa mhanga kwake ili nisafishwe na nitakaswe. Matokeo ya mabadiliko ndani yangu yatanifanya niwe " Nuru ya Ulimwengu". Sasa hivi, muundo wa maisha yangu utakuwa onyesho na kuwa ushuhuda wa kuonw3a na wote. Kwa hivyo msimamo wangu ni sharti uwe ule wa Yesu Kristo. (Wafilipi 2: 6 - 11).

Katika mwaka wa 1990 nilipo kuwa katibu wa Yearly Meeting yangu

nilipata fursa ya kufanya kazi na waakilishi wa Friends United Meeting (FUM) waliohimiza na kuwapa nguvu Marafiki wa Mikutano ( Makanisa ) yetu. Tulitembelea mikutano nyingi na tukakutana na waakilishi kutoka mikutano mingine. Mary Glenn Hadley katibu msaidizi wa FUM wakati huo, alitoa ujumbe wake wakati wa ibada ya asubuhi Jumapili kule Kingston. Msingi wa usemi wake uliegemea hadithi ya Yesu Kristo kuhusu kuvua samaki. (Yohana 21:1 - 14). Bwana wetu Yesu Kristo alimwamuru Petro naye Petro akaenda kwa utiifu, yeye Petro alifaulu. Siku hiyo Mungu alisema nami. Akasema, "Unapo chukua hatua ya imani nitafungua madirisha ya mbinguni na kukumwagia baraka zangu".

Katika mwaka wa 1991, nilipo kuwa nikitafuta uongozi wake Mungu ili nianzishe shule ya Biblia ya likizo katika mkutano wangu (Dover), Myra Brady ( Mmoja wa kikundi cha waakilishi wa FUM ) alijitoa kufungua shule ya Biblia kwa yearly meeting ya Jamaica chini ya udhamini wa yearly meeting ya Kaskazini Carolina. Julai 1992 shule ya shughuli ya Biblia iliendelezwa kwa mikutano minne. Huduma hii iliongezeka zaidi mwaka jana na tumekuza na kulisha zaidi ya watoto 2000 katika mikutano saba. Shule ya Biblia imekuwa jina la wenyeji wa jamii nyingi ambayo imefaidi watoto ambao kwa subira wangojea kubadilisha ratiba ya likizo yao kuweza kuhudhuria kipindi kijacho. Bwana wetu Yesu Kristo aliambia Petro, " Kama wanipenda lisha wanakondo wangu". Tunajaribu kufanya vivyo hivyo. "Jinsi hiyo hiyo, Mwana wa mtu hakuja kutumika bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi" (Mathayo 20:28).



Sala: "Bwana mpendwa, najitoa kuishi maisha yako. O! nitunze kila

siku, shahidi mwaminifu mwenye maish ya mapito yaliyombondeka. Nishike mkono wangu uniongoze kote unako nihitaji. Nilishe na Roho wako hata niwe salama nyumbani" (J.W. Gaines)



Maswali:

- Mwito wa kushuhudia huja kwako kwa njia gani?

- Twawezaje kushiriki na watoto wetu kwa maisha ya kuabudu?





Ushahidi kwa Uaminifu



Rachel Muers Britain Yearly Meeting

Nnapenda vifungu vya Biblia vinavyo zungumzia uaminifu wa Mungu kwa ulimwengu wake - uaminifu unaodumu hata ingawa ulimwengu hubadilika. Kuwa mashahidi waaminifu ni sehemu moja, nina sadiki, kuwa shahidi kwa ule uaminifu.

Kuwa shahidi kwa uaminifu wa Mungu huenda inamaanisha kujitayarisha kutenda kwa njia isemayo mwaka ujao, au miaka mia moja au elfu moja ijayo, ni ya maana. Maana nyingine ni kuwa tayari kungojea: kukataa nguvu za kitamaduni zisemazo, "cha muhimu ni kupata unachotaka sasa".

Ninapo fikiria kwamba maishani mwangu ni pahali pa "ushahidi wa uaminifu" kutendeka, nafikiria kwa mfano, kujihusisha na mambo ya muda mrefu ya miungano ya kujitolea: juu ya idadi inayoongezeka ya uharibifu wa mazingira maishani mwangu: kujiingiza katika uhusiano wa maisha ya muda mrefu. Ninapo mjua Mungu na ulimwengu hapana hata moja ya mienendo hii imefanyika. Pengine kulingana na kupanuka kwa hisia yangu kuhusu kuwa "Shahidi wa Uaminifu wa Mungu" kwa sehemu moja imetokana na maarifa ninayo kwamba mimi si mmoja wao wa Marafiki ambao kuelewa kwao kwa mambo ya kiroho hutambulika kwa "Kilele cha ujuzi" au muda wa mkazo wa dhihirisho.

Hii haimaanishi kuwa njia ya utambuzi si ya maana kwangu. Kawaida mimi si mtu mvumilivu, lakini inaonekana kwangu kwamba nina weza kuhudumia Mungu katika ulimwengu unaobadilika - kwa jumla mabadiliko haya ni upendo wa Mungu kwa ulimwengu, "kusudi" la uaminifu wa Mungu - nikiwa na uvumilivu wa uangalifu wa yale yanayo tendeka. Hii inasikika kwa urahisi. Kulingana na ujuzi wangu hii ni moja wapo ya vita vigumu kufanya. Kwa mawazo yangu ninajijengea miundo yenye majibu yasio fikiriwa: kuchukia watu, maneno au vifungu vinavyonifanya kutosikiza, kupendelea majibu ya maswali magumu. Katika ulimwengu uliotatizika wote twajaribu kurahisisha njia za uamuzi, kufanya tabia ili tusionekana kama kila chaguo ni la mara ya kwanza. Kuwa shahidi mwaminifu pia ni kubuni tabia ya kusikiliza. Mikutano ya ibaada ni ya muhimu, na tena kusoma biblia na hata njia za mafundisho kunionyesha kusudi ya upendo wa Mungu usio na kifani unao weza kunipa uvumilivu wa kusikiliza.

Maswali:

-Tunaweza kutambuaje kibinafsi au kama kikundi ni nini Mungu anataka tufanye?

- Twawezaje kuwa waaminifu kwa kila kitu kila siku?

Ujumbe wa Wakweka



Helmer Batista North Carolina Yearly Meeting (FUM)



Kulingana na neno la Mungu, Bwana atuambia kwamba tuwe mashahidi wake ulimwenguni mzima. Wakati Mungu alipo umba ulimwengu, haikukuwa nia yake kuweka mipaka ya kutugawanya. Alitamani maumbo yake duniani yawe yakufurahisha na yaweze kutunzwa nasi wanadamu kwa hekima na maarifa, kuistawisha thabiti ili ikamilishe madhumuni yake ya kuturuhusu kuishi pahali patakatifu patakapo tunzwa vyema.

Lakini wanadamu wameweka mipaka yakutugawanya kitaifa, kitamaduni, kilugha, kimaumbile, kisiasa na kiuchumi hata kimawazo. Zaidi ya hayo tumejigawa kwa makundi tofauti ya kidini. Haikukuwa nia ya Kristo kubuni dini. Kila mara alipinga kwa nguvu yote ya uongo katika miundo ya dini. Na hata haikukuwa wazo la George Fox kuanzisha dini. Kwa muda mrefu tumefurikwa, tumeambukizwa au tumechafuliwa na mawazo fulani ya kidini na kutuzuia tusijue maana na matendo ya Marafiki.

Tuna ujumbe mpya uliotoneshwa kutokana na biblia yenye ujuzi wa miaka mingi ya kuhudumu kupita mipaka ifunikayo mambo ya Kikweka. Huu ni ujumbe wa upendo, amani ya kindani, uhuru na kukubalika vilivyo dumishwa na Wakweka kwa miaka mingi. Mpangilio huu unatoa uhuru wa kukubalika kwa wale ndugu na dada wa mikusanyiko mingine bila kuwashurtisha kuachana na baadhi ya desturi zao za awali na wapewe nafasi ya kumukubali Roho Mtakatifu awaingie na awasaidie kuleta mabadiliko .

Sisi Marafiki inatupasa kutilia maanani wajibu wetu wa kuwasaidia wale watu ambao hawajamtambua Mungu, wale si Marafiki wa Kristo, wale hawaja kabiliana na Roho Mtakatifu, wajihisi kwamba puzio la Roho lawavutia kujiunga na ujuzi wa kipekee wa ukombozi una wafanya wapya, si kwa nguvu zao bali wamejiruhusu kufanywa wapya na Mungu.

Hakuna mipaka kwa ufahamivu wa Mungu, iwe ya kidunia, kisiasa, kitamaduni, kiuchumi, kidini na hata aina nyingine yoyote. Kuna wanaume na wanawake wenye haja ya kibinafsi ya maarifa ya Mungu, wenye njaa ya kibinafsi ya kukabiliana na Mungu, wanao tarajia kupata ukweli na unyofu wa miale ya nuru. Wanaume na wanawake hao hufanya kazi, husafiri, huota na hua na muamko wa ukweli kwamba elimu ya kiufundi, sayanzi, maarifa ya mwanadamu, elimu ya utu vimetimiliza haja fulani, lakini haja za kiroho zinazo tupatia nguvu za ustahimilivu wakati wa majaribio, hutupa tumaini na kutujaza na furaha ya siku za usoni, hutupa tegemeo la kibinafsi kwa Mungu kupitia kwa Kristo na usaidizi wa Roho mtakatifu.

Wandugu na wadada hili ni jambo kubwa. Wafanya kazi ni wachache na mavuno yatayari, mawazo na mioyo ya wanaume na wanawake yatayari kupokea mbegu ya injili. Matukio ya mwongo uliopita yametuelekeza kwa uhakika huu. Zaidi na yale ya hapo awali,leo, watu wanahitaji maarifa, maarifa yasiyo na masharti ya kidini wala sheria za kidini yanayoweza kuwatenganisha na ukweli wa Mungu asemaye, "Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha". Tunapoelekea kwa wakati ujao usioeleweka, neno la Bwana latwambia, "Sitamuacha kamwe. Nitakuwa nanyi hadi mwisho wa dunia". Marafiki yatupasa kukumbuka maneno alipoambiwa Yoshua yenye umuhimu nyakati za Waebrania: "Msiche, wala msifadhaike, iweni hodari na mioyo ya ushujaa" (Yoshua 10:25)

Maswali:

- Kukutana na Mungu uso kwa uso kuna maana gani kwako?

- Makanisa yetu na mikutano yetu ya Marafiki yana uhakika gani kwamba utaratibu wetu haupingi bali watangaza ukweli wa ujmbe wetu?

Ukweli usiobadilika



Phyllis Short Aotearoa/New Zealand Yearly Meeting

Aotearoa, hutamkwa "ah-oh-te (kama tent kwa kingereza) -ah-ro-ah", ni jina la kienyeji la wamaori kumaanisha New Zealand. Neno hilo linamaanisha "Ulimwengu (au ardhi) ya wingu refu jeupe". Jina hili ni la kawaida kwa matumizi ya kisasa.

Sisi hapa Aotearoa/New Zealand tukiwa wa jamii ya Marafiki wa ulimwengu mzima tu upande wa kusini ya mwisho. Hapa jua huzungukia kaskazini wakati huo sisi hua na msimu wa kiangazi na hali nusu ya kaskazini mwa dunia kuna msimu wa baridi kali. Iwapo hivyo, hapa "pembe ya mwisho ya dunia", Roho ya ndani yetu, "watu wa mwanzo", Wamaori, wale wa asilia ya Waingereza na wakisasa, wahamiaji wa mataifa mengi.

Tunapokiri Roho ama Nuru yu ndani mwetu, tu tayari kupokea nguvu za kuishi kama mashahidi wa uaminifu. Marafiki ulimwengu wote wana umoja wa kukumbatia watu wote.

Kwa uhai wangu wote nimekadiria thamani ya urithi wa ukristo na mizizi ya Ukweka: maisha na mafundisho ya Yesu yanayo tuongoza na nuru iangazayo hata baada ya miaka 2000: na kutokana na utambuzi wa George Fox wenye maarifa kwamba Kristo ni mwalimu wa kindani na Roho au Mungu huishi ndani ya kila mwanadamu. Kutoka kwa ukweli na maarifa ya Marafiki ya karne nyingi kumejitokeza ushuhuda wa Kikweka kuhusu usawa, amani, uadilifu na dhahiri. Nimevutiwa na waume na wake ambao wamekuwa waaminifu kwa ukweli huu.

Katika Aotearoa/New Zealand "nabii" wa Wamaori kwa jina Te Whiti, alitumia kanuni za ukristo alizokuwa amejifunza. Mwisho mwisho wa karne ya kumi na tisa aliongoza watu wake kwa matendo ya maombi na amani kujaribu kuokoa inchi na kijiji chao kutoka kwa utawala wa Waingereza. Waliomba, wakaimba nyimbo, mbele ya vikosi vya majeshi, waliendelea na kulima mashamba yao, watoto walileta maua na kupatia askari.

Nilipokuwa India kwa ibada ya Wakweka, maajabu nilitarajia kwa safari hii ni kukutana na Gandhi akiwa mahali pake pa ibada. Huyu mtu alikuwa na kiasilia ya Kihindu na alikuwa mwenye sifa sana na ambaye alivutiwa na rafiki zake wakristo, waliojumuisha Wakweka, alinionyesha kwa uso wake Yesu alikuwa wa namna gani. Hii ilidhihirishwa na upendo mkuu Gandhi alikuwa nao kwa maskini na uwezo wake wa kuitikia mara moja kwa mahitaji ya wale walio mjia na "kusema ukweli kwa utawala". Sifa hizi pamoja na maombi ya kila mara na kufunga akitafuta uongozi wa mambo ya mbele ilimvutia sana.

Watu kama hawa ambao hutenda mema siku baada ya siku na katika hali tofauti kuonyesha upendo na kufanya kazi ya haki na ukweli huinua roho yangu sana. Ninajua, katika hali na wakati wa mabadiliko, ni lazima kupitia kwa sala na maombi nitafute uongozi wa Roho leo hii, na kujiunga na Marafiki wengine kujifunza kuishi pamoja au peke yangu kwa ukweli usiobadilika ambao tumepewa.

Maswali:

- Ni ukweli gani usiobadilika katika maisha yako ya kiroho? Unawasiliana vipi na wenzako kuhusu haya?

- Unaweza kupateje wale watu wakukuvutia?



Thibitisho



Susannah Brindle Australia Yearly Meeting



Tukitazamia kushuhudia kristo roho ndani yetu kwa ulimwengu usiobadilika na uliochafuliwa nina thibitisha:

Kwamba Mungu - msingi wa uhai wetu - ni Mungu wa ulimwengu,wa juu mbinguni,na vyote vya uhai chini ardhini, ni Mungu wa viumbe vyote vya majini na chini ya kilindi, kuchomoza na kutua kwa jua kali, wa upepo uvumao na hewa ya utulizo, kama, "kile cha Mungu" kipatikanacho kwa kila mtu kipulizacho pumzi ya uhai wa roho. "Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote" (Ayub 12;10).

Kwamba tunapo dhuru mdogo mmoja apo wa wale ndugu zetu, huwa tumedhuru wote. Kwamba Roho wa Kristo aishiye ajulikane kamili kwa yote tukijua hatuko peke yetu "niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?" (Zaburi 139:7).

Kwamba wajibu wetu kama wakristo ni kuwa upendo wa dhahiri tena sawa kwa maisha yote ya Mungu.

Kwamba kutokana na mjadala huu wa kwanza wa upendo wa ulimwengu uwe mwanzo wa ushahidi wetu kwa amani, uaminifu na usawa wa ukoo wa wanadamu na hata kupita uanadamu duniani (kupita uanadamu humaanisha "vyote visivyo wanadamu" pamoja na utu utakao jitokeza), na huu upendo wa ulimwengu utatuongoza na kukudumisha.

Kwamba upendo huu ni wa kujifunza na wala si elimu tupu au madhanio, lakini ni kwa maarifa ya hakika kamili ya mapenzi ya ushirika wa walio na upendo.

Kwamba kujua na kupenda uumbaji lazima kujua kiini kwa wingi na umoja wa usemi - "lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; na ndege wa angani, nao wata kuambia; au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia. "(Ayubu 12:7-8) - tutagundua mpigo wake ni mpigo wetu na roho yetu, mpigo na roho ya mungu.

Kwamba uumbaji wa ukoo, tuliojifunza kutoka kwa watu asili wa ulimwengu unaoweza kutuelekeza kwa unyenyekevu kujitoa kwa uongozi wa roho kwa uhai wote.

Kwamba ni kwa uongozi wa wale ambao yote ni ya Mungu unaoweza kukurejesha kwa ushirika na wale tulio kuwa tumepuuza hapo awali kwa kuwa tulijiona kuwa bora zaidi, na kuharibiwa na hofu ya kumalizika kwetu.

Kwamba kupitia kwa nuru ya uumbaji, ambayo Mungu aliita njema, tukome kuogopa sehemu za kivuli, hadi sasa inayo hisiwa "kupitia kioo cheusi"

Kwamba tukifanya hivyo tutakuja kushuhudia waaminifu kwa kumtumikia Mungu katika ulimwengu unaobadilika.

Swali:

- Tunaweza kujifunza vipi kuuchukulia ulimwengu wote kuwa uumbaji wa Mungu?



Moto Mioyoni mwetu

Diego Chuyma INELA Bolivia

Katika ulimwengu unaobadilika huu tuna hitaji masharti matatu; kumjua Kristo aliye fufuka, kijazwa na Roho Mtakatifu na kuwa mashihidi waaminifu. Kwanza, kumjua Kristo aliye fufuka hasa, si kumjua tu Kristo bali ni kumjua kiasili. Yeyote aliyemjua Kristo si yule yule. Kabla mtume Paulo kuwa mwongofu alikuwa kiongozi wa dini; alijua biblia na mafundisho yake, lakini hakumtambua Kristo na nafasi zake. Alipo kutana na Kristo njiani kwenda Dameski, maisha yake yalibadilika kabisa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kuwa na George Fox. Pili, masharti ya kujazwa na Roho Mtakatifu (Luka 11: 9-13). Yatupasa tuendelee na kujazwa na Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18). Tatu yatupasa kufahamu msimamo wa kuamua kwetu kuwa mashahidi wa Kristo. Sababu ya kuishi kwetu iwe ya kueneza injili.

Kuwa mashahidi wa Kristo wa kufaa, tuahitaji kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Yesu alihitaji upako wa Roho Mtakatifu ili aweze kutenda kazi njema (Matendo 10:38). Alisema tungefanya mambo aliyoyafanya na hata makuu zaidi (Yohane 14:12). Kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kunalete mabadiliko ya maisha, maisha matakatifu na maisha ya ushindi kwa jamaa, jamii, miji mikuu na hata ulimwengu wote.

Twapokea Roho Mtakatifu kutenda kazi ile ya Yesu, kuwa kanisa la ujumbe. Marafiki kutoka kote ulimwenguni, zaidi mno twahitaji ujumbe wa jitihada, juhudi kwa roho zilipotea. Ulimwengu utayari kumpokea Yesu na kubadilishwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Ufufuo unaendelea na watu wanaendelea kuokoka. Kama Marafiki tuwe pamoja kwa kukusanya roho hizi kwa Yesu. Kama watu wa Mungu, tuwe mabalozi wa Kristo kwa ulimwengu huu unaobadilika. Wako wapi wale "mashujaa sitini"walio kuwa na jitihada za kubadilisha ulimwengu kwa Yesu Kristo? Yesu alituamuru tuenende tukawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi (Mathayo 28:19-20). Tukizipokea nguvu za Roho Mtakatifu zitatufanya tuwe mashahidi wa nguvu nyumbani mwetu, nchini mwetu na hata mwisho wa ulimwengu. Tukiwa Marafiki wa kutii amri za Kristo (Yohane 15:14), tusifanye tu waongofu bali pia wanafunzi.Gharama ya kazi hii ni kuwa na moto mioyoni mwetu.

Maswali:

- Umepokea nguvu kupitia njia gani?

- Twawezeshwa vipi kubadilisha ulimwengu?

Ushahidi



Anne Thomas Canadian Yearly Meeting



Nilipokuwa ni kitembea mle nyumbani mwa Marafiki, Toronto ilijulikana kwangu kwa ghafula kwamba singaliweza kulipa ushuru wa vita. Kulikuwako na kundi dogo la Marafiki kutoka Mkutano wa Canadian Yearly Meeting lilokuwa liaminifu ambalo lilikuwa limejizuia kulipa ushuru wa vita kwa miaka mingi, ingawa niliheshimu ushuhuda wa Marafiki hawa hadi wakati huo, jambo hili nililiona halikuniruhusu. Kuhusu uongozi wangu nilijihisi kuwa mwepesi na kuonekana wazi kamili. Miaka yote niliyo dumisha ushahidi huu uwazi huu haukuniacha kamwe.

Niliporudi nyumbani nilizungumza na mme wangu na watoto, waliofikiria kwamba huu ulikuwa upuzi. Hata hivyo, ni kiasi gani cha pesa ningaliweza kuhifadhi kutokana na kazi yangu ya muda ya daraja ya Kikweka? Hii ingalikuwa na faida gani? Ingaliweza kuhatarisha hazina zetu za kijamaa?

Na hii ingalifanywa je? Kufikia wakati huu wasusiaji wa kulipa ushuru kule Canada walikuwa ni wale wakujiajiri, kwa kuwa hakuna muungano wowote ulioweza kukubali kuvunja sheria ya ulipaji ushuru kwa niaba ya wafanyi kazi wao. Nilizungumza na mkutano wangu wa mwezi ulio buni kamati ya Uwazi kukutana nami. Wana kamati walionyesha uwazi kwamba hawakuelewa "mfano wa ishara". Tulikutana mara nyingi sana na kamati ikaarifu Mkutano Wa Mwezi kwamba, hata ingawa hawakuunga mkono ushindani wa kutoza ushuru wa vita, walitambua ya kwamba uongozi wangu ulikuwa wa kufaa.

Niliarifu mkutano wa Yearly Meeting kuhusu uongozi wangu na nikawauliza, wao kama waajiri wangu, kama wangeweza kusimamisha kulipa kiwango cha asili mia cha ushuru kwa vita vilivyopo na vile vilivyo pita, kadiri ya asili mia tisa ya mapato yangu. Yearly Meeting ilibuni kamati na kutafuta ushauri wa kisheria kuhusu ni nani ange ajibika ikiwa serikali ingeamua kupokonya fedha zilizo shikiliwa na muungano na kupigwa faini. Baada ya miaka mitatu Yearly Meeting iliidhinisha muhtasari wa majadiliano na kuunga mkono wafanyakazi waliokuwa wamepinga utoaji wa ushuru wa vita, mwajiri wa kwanza na wapekee wa Canada afanye hivyo.

Nilipowasilisha ushuru wa kila mwezi vile ilitakikana, nilifatisha barua ya kueleza hali ya upunguaji na pia kujulisha serikali jina la banki na nambari ya akaunti nilipoweka dola za kimarekani kumi na tatu $13. Barua ya kila mwezi ilikuwa na aya ya usemi tofauti kuhusu ushuhuda wa amani. Wafanyakazi wengine wa Yearly Meeting hawakukuwa na mwito huu wa uongozi, ili-nilazimu kufunga akaunti hiyo nilipo jiuuzulu wadhifa wangu miaka mingi baadaye na nikatuma pesa hizo kwa Canadian Friends Service Committee na nikajulisha serikali juu ya jambo hili.

Ilistahili? Ninaamini hivyo. Sikuwa na lingine la kufanya.



Maswali:

- Ni ujuzi upi umewahi kuwa nao unapo ongozwa na mwito wa kutenda jambo Fulani la ushahidi kuhusu uhusiano wako na mambo ya kidunia?

- Twawezaje makanisani mwetu na mikutanoni mwetu kuwasaidia wenzetu kujaribu miongozo yetu?

Kutaaznga habari njema



Dan Cammack North West Yearly Meeting

Mwaka 1647 George Fox alisikia maneno haya: Kuna Mungu mmoja hata Kristo Yesu, ambaye anaweza kuzungumza kuhusu hali yako; Moyo wake ulirukaruka kwa furaha, hivyo Fox alianza kutangaza habari njema ya Yesu kwa watu wa Uingereza wa wakati ule. Ghafla taarifa ilianza kuenea kwa nchi za karibu (zilizoizunguka) na za Amerika. Maelfu ya watu waliitikia na hivyo kuyainua macho yao kwa Yesu, wakiyaelekeza masikio yao ili kwamba waisikie sauti yake kwa utii wakiendelea kumfuata.

Katika karne zilizofuata Marafiki waliendelea kuipeleka Habari Njema ya Yesu ulimwenguni kote. Baadhi ya watu wa familia yangu walikuwa sehemu ya wale waliohusika kuuchukua ujumbe kwa watu wa Aymara katika milima ya Bolivia na Peru.

Helen Cammack, shangazi yangu mkuu alikuwa miongoni mwa kundi la awali kwenda Bolivia linaloitwa kwa sasa North West Yearly Meeting (USA). Helen, Seja na mkufunzi, alifika La Paz mapema katika mwaka wa 1930. Kufuatana na uhaba wa barabara na magari, Helen alipata nyumbu aliyeitwa Binti mfalme. Muda wake mwingi aliutumia kuanzisha shule karibu na ziwa Titicaca. Pia alianzisha ukusanyaji wa maneno ya Aymara na hivyo kumwezesha kuunda kamusi. Si chini ya mara moja wakati wa usiku Binti mfalme alijihisi mlegevu. Helen angeweza kuamuka na kuzunguka nchi nzima au sehemu zote akimtafuta nyumbu wake kaidi.

Kwa kutembelea Pacific North West Helen alihubiri ujumbe katika

Yohana 12 :24 kimsingi yakiwa maneno ya Yesu."Kweli nawambieni punje ya ngano hubaki ngano tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa kama ikifa huzaa matunda mengi". Baadaye katika mwaka wa 1944, Helen alifariki kwa ugonjwa wa homaya manjano huko La Paz. Kulikuwepo mamia kadha ya Marafiki huko Bolivia kwa wakati huo.

Sasa ni 2002 mimi pamoja na familia yangu tunahitimisha miaka kumi na nne (14) ya huduma ya kimisionari nchini Peru. Kwa muda wa juma chache tutapanda matatu - DalaDala safi tukielekea huko La Paz. Kando kando ya njia tutaona majumba mengi ya mikutano. Tutapanda kupitia sehemu ambayo binti mfalme alijificha na akitafutwa na shangazi mkuu Helen. Tutakapokuwa tumeingia ndani ya ndege tayari kwa United States, tutakuwa tukikumbuka kiasi cha Marafiki 10,000 ambao wanaunda mikutano ya mwaka ya Peru pia Bolivia (Yearly Meeting of Bolivia na Peru).

Asante Yesu kwakuturushusu kutupa kibali cha kutangaza Habari Njema.

Maswali:

- Unafahamu nini kuhusu kutangaza Habari Njema?

- Unaitikiaje kuhusu ukweli huu ambao Fox alisema ya kwamba kuna mmoja Kristo Yesu, angaliweza kusema juu ya hali yake?



Kesha kwa Amani



Misha Roshchin Mosco Monthly Meeting



Wakati wa masika mwaka wa 1999 ulikuwa wa baridi sana. Kufikia mwisho wa mwezi wa Oktoba ghathabu ya vita vyapili vya Chechen ilikuwa inaendelea. Wakimbizi walikuwa wakitiririka kutoka Chechnya, lakini kule Moscow kulikuwa kutulivu na kwa amani. Wakati huu hakuna yeyote aliye kuwa akipinga vita - wengi walikumbuka milipuko iliyo kuwa kule Moscow, na wengi walihakikisha kwamba Wachechen wana lawama. Wakati huo wachache sana waligundua kwamba taifa lilikuwa limekumbwa na msiba wa kushinda, na hata njia ya mtiririko wa damu haukulenga uelewano mwema kati ya Warusi na Wachechen.

Mashaka ya shughuli kubwa nilikuwa nayo ilinigusa sana kwa sababu singeweza kufanya lolote. Nilimpigia simu Viktor Popkor, mtu wa imani ya ndani na Muumini wa kale. Wakati wa vita vya kwanza vya Chechnya Viktor alikuwa na bidii kwa kazi. Aliweza kuingiza misaada ya kibinadamu, akapanga ubadilishanaji wa wafungwa na akawa mtazamaji wa makubaliano mafupi ya kusimamisha vita wakati wa msimu wa kiangazi mwaka wa 1995. Wakati huu wote tuligundua ya kwamba hatungekuwa na wingi wa kupinga vita. Kilio cha waandishi wa habari kilikuwa "Wacha jeshi letu likamilishe kazi yao". Hakuna yeyote aliyeweza kutoa maelezo kamili ya msemo huu.

Viktor alipendekeza mgomo wa kususia chakula kwa umoja wa amani na watu wa Chechenya. Kususia kwetu kwa chakula kuli kuwa kufunga halisi kwa maana kila mara tulikuwa tukinywa maji moto kwa jumba la karibu lilokuwa ni la MEMORIAL,(ukumbusho) muungano wa haki za binadamu. Kwa fumbo letu la maneno tulichagua maneno ya mfalme wa zama za kale wa Rusia aliyejulikana kama Alexander Nevsky: "Si kwa nguvu eeh Mungu bali kwa ukweli" kitendo chetu kilianza kando ya jiwe la Malo Solovetsky lililoletwa kutoka Solovki, ambapo kambi ya wafungwa wa kisiasa ilisimamishwa wakati wa Stalinist. Karibu na jiwe Solovetsky tulijenga hema la makaratasi. Pale, kwa meza ya kukunja tuliweka vitabu vya sanamu. Tuliombea wale walio potea kwa vita - Wachechen na Warusi, Wakristo na Waislamu.

Tulieleza tulilokuwa tukifanya - na kwa nini - kwa yeyote aliyekaribia. Ningependa kusema wote tulipata msaada kutoka kwa wengi. Ninafahamu hasa mwanamke mmoja aliyesafiri kutoka mji mwingine kwa minajili ya kukutana nasi.

Siku tisa kutangulia mgomo wetu wa kususia chakula nafasi yangu ilichukuliwa na rafiki yangu Sasha Gorbenko, mshiriki wa Mkutano wa Mwezi wa Moscow. Alisusia chakula kwa siku 43 hadi uchaguzi wa Russian Duma uliofanyika. Sasha aliitikia mwito wa kujitolea kwa kiroho wa hali ya juu wakati wa umwagikaji wa damu na watu wasio na hatia wakifa. Matokeo ya kazi yetu yalikuwa haba sana, hata hivyo ilikuwa hima kufanya jambo Fulani badala ya kuketi kimya na hali uhalifu waendelea kufanywa kwa kusingizia Warusi wote.

Baada ya kususia chakula kwa muda wa wiki tano mfululizo Viktor Popkor alisafiri kwenda Chechnya kuhudhuria mkuatano na raisi wa inchi hiyo, Aslan Maskhadov. Ilikuwa mawazo ya Viktor kwamba mkutano huo ungesimamisha vita. Wachechen walimpokea huyu mtu wa imani tofauti na mwenye nia njema kwa heshima. Aliweza kufikia vijiji vya Urus- Martan na Valerik, lakini hakuweza kuvuka mpaka na kufikia jimbo la utawala wa majeshi ya muungano. Wakati wa majira ya baridi ya mwaka 2000 Viktor aliweza kufikia Chechnya mara mbili. Alibeba pesa, akanunua unga wa kugawiya wana vijiji. Mwisho, aliweza kukutana na Raisi Aslan Maskhadov, wakati wa majira ya chimbuko, lakini mwendo wa kufikia amani ukawa mgumu kuliko tulipotarajia. Vita vya kila siku hupanda mbegu mpya ya chuki.

Tarehe 18 Aprili 2001 Viktor alipata majeraha ya kifo kule Chechnya, sio mbali kutoka Grozny, kutokana na wapiga bunduki wasiojulikana. Aliaga tarehe 2 Juni 2001. Maishani mwake alijaribu kumtumkia Mungu wakati huu mgumu. Alikuwa karibu sana na Mkutano wa Mwezi Moscow. Wachache wetu Marafiki kutoka Moscow tulijitahidi kuleta amani.

Ninasadiki kwamba tukirarua chuki kutoka mioyoni mwetu tutaweza kukutana na wenzetu. Ni wakati huo tu tunaweza kujua hamna la wema zaidi kuliko amani.

Maswali:

- Katika ulimwengu wa udhalimu na ubadilifu kuna maana gani kutafuta amani?

- Twaweza kuishi namna gani maisha ya amani?





Ushuhudiaji wa Ki-Imani



Kenneth Co Hong Kong Monthly Meeting



Ni kipi wa Quaker wasio waongofu wa kadiri watakachokifanya kwa ulimwengu unaobadilika ili wawe washuhudiaji wa kweli? Tukiwa wanaume na wanawake wa imani tunalazimika kujua nini maana ya kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote na kuwapenda jirani yetu kama tujipendavyo. Kwa maneno mengine, lazima tujue uwepo wa Mungu una maana gani katika maisha yetu, itikadi zetu kumuhusu Mungu zinakuwa hai pale tu tunapoendelea kupambana kila siku kimaisha na kifo. Kama watendaji wa imani na ushuhuda, lazima tuwe watu wenye mtazamo usio wa kawaida wa kuona mambo yakitokea katika dunia, watu wale ambao chapa ya Yesu ni maana kwa sababu tunatakiwa kufuata mfano wake na kumuishia.Kumfuata Yesu ni kuishi katika Nuru ya upendo; tunahitajika kushirikisha nuru hii tulioipokea kwa ulimwengu.

Kuwa washuhudiaji halisi maana yake kuyaweka kivitendo yale tuyaaminio. Ingawaje, "The Religious Society of Friends" haina (creeds) Lakini tunazo shuhuda. Haya ni pamoja na kuambiana ukweli; kuamua kuishi maisha ya amani na Yesu na yasio ya kikatili na ya kujikana.

Kujikana kunamaanisha kuviweka baadhi ya vipaombele tofauti au taratibu katika maisha yetu. Kuurahisisha mfumo wetu wa maisha ili kwamba kile ambacho ni muhimu zaidi - ni kuwa karibu na Mungu na kufahamu ni nini mpango wa Mungu katika maisha yetu na hivyo kutenda kulingana na taratibu hizo - mara moja. Kusema kweli kuna maana ya kuendelea kuambatana na kweli hata kama wakati mwengine inaweza kutufanya sisi tusionekane watu maarufu, kupoteza yale ambayo tunafikiria kama baraka au mfano ama kutuweka katika hali dhiki.

Mwisho kuishi maisha ya amani na yasio ya kivita au mapambano si jambo jepesi lazima li gharimu, hasa baada ya September 11 2001 wakati wanenaji mahiri wa kidunia walijaribu kulinganisha uzalendo na wema na hivyo kutangaza dhidi ya mafundisho yaliyokwisha simamishwa au jengwa inaonekana kama si kizalendo na kwa hivyo kuwa sambamba au kuambatanishwa na uovu. Mojawapo wa wanachama wetu, Steven Palmquist, aliye andika nakala hivi karibuni katika jaride au gazeti la "The South China Morning Post:"

Si vema kuzungumzia kama watu punguani juu ya ugaidi kana kwamba kuufutilia mbali kutaleta amani - lakini ni pale tu ugaidi wa mwanadamu iliyohuhikiwa kwa mifumo yote ya nguvu utakapotatuliwa. Kutatua migogoro kwa nguvu maana yake halisi ni uendeleshaji wa uharibifu wa pande husika za kibinadamu….. taratibu kama non-violence si uzuri ni fikra zisizotendeka, ni hoja zenye nguvu pale tu tunapoziishia. Watu wengi wanapoziishia ndiposa matumaini ya kupatikana kwa amani ya kudumu yawezekana.

Zipo njia nyingi sana kuwa washuhudiaji halisi. Nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa daktari ambaye alipotimiza miaka hamsini (50) aliamua kuacha huduma ya kitabibu huko Seattle na akaamua kufanya kazi ya umishenari kama sehemu ya maisha huko China, akiwafundisha wenyeji wa China hasa watumishi wa kanisa ili wawe viongozi wazuri wa kundi la kujifunza neno au Biblia. Rafiki yangu mwingne aliye hitimu na kupata shahada ya Master of Divinity anaacha nafasi nzuri aliyonayo kama mkufunzi na kujiunga na Amity Foundation kama mkufunzi wa kujitolea sehemu za mashambani au vijijini huko China.

Hii yote ni mfulilizo wa mifano inayotuwezesha kuendelea kusikia kwa utulivu wito wetu. Haijalishi ni kwa njia gani kila mmoja wetu alivyoitwa, jibu tunalipata kwa kusikia sauti ya ndani, maisha ya kujidhabihu yanayomfanya mtu kuondoka na kuhudumia kwa furaha ulimwengu kote, akikutana na hitaji la Mungu kwa kila mmoja.





Maswali:

- Tunafanyaje tunapozungumzia juu ya ukweli na tunapoziacha kanuni kama Quaker katika maisha yetu ya kila siku?

- Ni kwa jinsi gani tunawezungumzisha juu ya kweli wale walioko katika nyazifa na madaraka ya kiutendaji?

Misingi wa Ushuhuda Mtilivu Kujenga



Val Liveoak South Central Yearly Meeting



Mara nyingi nimejisikia mdhaifu ninapo jaribu kusema Ukweli mbele ya wenye nguvu duniani. Ninapo kumbuka ushuhuda mwaminifu wa Marafiki wa Kizazi kilicho nitangulia, mara nyingi huwaza, "Ni nini walichokuwa nacho ambacho sina?"

Baada ya muda kidogo nimekuja kugundua baadhi ya yale Marafiki wa hapo awali walijua. Nilirejelea Marafiki baada ya kutafuta kwa muda mrefu haki za kidini, nilikuwa nimesoma Biblia hadi kiwango fulani, lakini kama Rafiki asiye na ratiba nimekuwa na wakati mchache wa kuisoma.

Mbali na ufahamu wa hali ya juu wa injili, hivi juzi juzi nime shutuliwa na uwezo wa lugha ya wa nabii wa Kihebrania, na nimekata kauli kujifunza upana wa chanzo cha nguvu na neema ya Mungu.

Ninaona haja ya kuongeza nguvu ya kuishi kwa maombi, kustawisha nafasi ya kuwasiliana na Mungu kwa ukimya dhidi ya kelele nyingi za ulimwengu wa sasa. Ni vigumu sana kwangu kukuza maadili haya hata hivyo uwezo wangu usio na msingi dhabiti na haba tena kavu.

George Fox na wenzi wake shujaa sitini waligundua vile ya kushirikiana kutafuta na kutenda uwepo wa Mungu. Kazi yangu na makundi ya Marafiki wa Amani ilikuwa kushiriki kwa uongozi wa Roho. Mimi kama mshirika wa tamaduni ya ubinafsi, hili limekuwa funzo gumu. Ujuzi mwingi ninayo kuhusu nguvu za utendaji zilizomo ushirika wa ugunduzi wa Marafiki, unanifanya nijue wajibu wangu wa kujenga mkutano wa jamii wa maombi ya kungojea uongozi wa Mungu kwa uamuzi. Uhusiano kati ya mizizi ya kazi na matunda ya maendeleo ya miradi yetu Afrika na Columbia imedhihirika.

Matendo rithishi kutoka vizazi vya awali yatakiwa kufufuliwa na kusafishwa kutupatia imani na uwezo wa Marafiki wa kale. Kazi yetu inapoendelea, ni maombi yangu tujifunze kutafuta uongozi wa Mungu wenyewe, kama kikundi na kwa maandishi, na hii itatupa nguvu zilizo zungumzwa kwa Matendo 1: 8



Maswali:

- Huwa unafanya nini unapo jisikia mnyonge kuitika kwa mwito wa Mungu? - Kuwa shahidi mwaminifu chanzo cha nguvu zako ni nini?